MANCHESTER CITY ANYAKUA UBINGWA WA EPL 2023/2024
Klabu ya Manchester City imetwaa Ubingwa wa English Premier League (EPL) baada ya kuifunga klabu ya West Ham United magoli 3-1 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba kombe hilo kwa mara nne mfululizo bila kupokeza kijiti hiko kwa klabu nyingine.
Manchester City inachukua ubingwa baada ya kufikisha pointi 91, ikifuatiwa na klabu ya Arsenal yenye alama 89 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Everton katika michezo ya kukamilisha msimu wa 2023/24 Mei 19,2024