WANANCHI WAMETAKIWA KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Wanawake wenye umri kuanzia Miaka 18 hadi 69 wametakiwa kujitokeza kwenye upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi katika Hospitali ya Mnazi Unguja Mmoja na Chakechake Kisiwani Pemba
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Amour Mohamed Suleiman alipokuwa akizungumza na Timu ya Madaktari kutoka China wanaotarajiwa kuanza zoezi la upimaji wa Saratani ya shingo ya Kizazi hapa Zanzibar.