MASHEHA NA MADIWANI KUYASIMAMIA VYEMA MAENEO YAO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ ,Mhe Masoud Ali Mohamed, amewasisitiza Masheha na Madiwani kuyasimamia vyema maeneo yao, ili kuimarisha ulinzi na usalama katika shehia zao.
Akizungumza na masheha, madiwani na Watendaji wa Wilaya ya Kusini huko Makunduchi, amesema kuwepo kwa Mikakati imara watakayoyaanzisha kutasaidia pia kuvidhibiti Vikundi vya uhalifu na Wananchi pamoja na Wageni wataendelea kuishi katika hali ya usalama.