VIFAA VYA KUSHUSHIA MAKONTENA VYAWASILI BANDARI YA MALINDI
Shirika la Bandari Zanzibar limesema tayari wameshaanza kutatua matatizo yanayolikabili hasa kwenye sehemu ya kushusha mizigo.
Akizungumza baada ya kupokea Vifaa vipya vya kubebea mizigo huko Malindi Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Akif Khamis amesema Mashine hizo zitawezesha kutatua matatizo yanayolikabili Shirika hasa kwenye sehemu ya kuchusha mizigo.
Amesema Vifaa hivyo vina uwezo mkubwa wa kushusha Makontena katika muda mdogo zaidi ukilinganisha na vilivyopo sasa.