WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUHAMIA MASOKO MAPYA YATAKAPOKAMILIKA
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mh Masoud Ali Mohammed, amewataka Wafanyabiasha waliopo katika Masoko ya muda, kuhamia katika Masoko mapya mara yatakapokamilika kujengwa.
Akizungumza na Kamati ya Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe ambayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni, ameagiza kupewa kipaumbele katika masoko mapya Wafanyabiasha waliokuwepo hapo awali na kufanya utaratibu wa kuwapatia nafasi Wafanyabiashara wengine.