WANANCHI WAMETAKIWA KUHUDHURIA SALA NA BARAZA LA EID
Ofisi ya Mufti Zanzibar imewaomba Wananchi kuhudhuria katika Ibada ya sala ya eid na baraza la eid ili kusikiliza nasaha na Miongozo itakayotolewa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussen Ali Mwinyi.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Khalid Ali Mfaume amesema Siku ya Eid ni muhimu kukumbushana mambo yanayohusu Dini ya Kiislamu na kukatazana mabaya ili kuepusha Jamii kwenda kinyume na Maadili yao