UCHUMI WA ZANZIBAR UMEIMARIKA KUTOKA TRILIONI 3 NUKTA 116 MWAKA 2020 NA KUFIKIA TRILIONI 3.499 MWAKA 2022.

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Katika Hutuba Yake Kwa Umma Usiku Wa Kuamkia Kilele Cha Mapinduzi Amesema Ongezeko Hilo Limechangiwa Na Masuala Mengi Ikiwemo Uwekezaji.

Hata Hivyo Ukusanyaji Mapato Nao Umeongezeka Kufikia Trilioni 1.4 Mwaka 2022/2023 Kutoka Bilioni 790.48 Mwaka 2020/2021.

 

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALI MBALI WALIOTUMIKIA SERIKALI KWA MIAKA KADHAA.

Sherehe Za Kuwatunuku Nishani Viongozi Hao Zimefanyika Katika Viwanja Vya Ikulu Mjini Zanzibar Katika Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Mwinyi Amemtunuku Nishani Ya Mapinduzi Ya Kiongozi Mwenye Sifa Ya Kipekee Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Nishani Nyengine Ni Viongozi Na Wananchi Wenye Sifa Maalum Ambapo Dkt Muhamed Gharib Bilal, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Seif Ali Iddi Na Marehemu Seif Sharif Hamad Wamekabidhiwa Nishani Hizo.

 

SERIKALI INA KILA SABABU YA KUFANYA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA BAHARINI ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA USAFIRI WA BAHARI

Ameyaeleza hayo Rais Wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Ambae Ameshuhudia Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Wa Bandari Ya Maruhubi Ikulu Zanzibar, Amesema Serikali Imeamua Kujenga Bandari Ya Maruhubi Kutokana Na Bandari Ya Malindi Kuzidiwa Na Abiria Pamoja Na Mizigo Na Kusababisha Msongamano.

Amesema Mradi Huo Utakuwa Mfano Mkubwa Wa Ushirikiano Wa Sera Ya Serikali Na Sekta Binafsi Ya PPP Katika Kufikia Malengo Ya Utekelezaji Wa Miradi Mbalimbali Nchini.

Subscribe to RAIS MWINYI
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.