KANDA YA ZIWA WAFIKIWA NA HUDUMA YA MAGONJWA YA MOYO
Zaidi ya Watu Milioni 22 wa Kanda ya Ziwa wamerahisishiwa huduma ya Magonjwa ya Moyo na matibabu ya kibingwa kufuatia Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Hospitalini hapo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi, huku akiweka bayana lengo la kuanzishwa kwa Hospitali hiyo.