WALIMU WA MADRASA KUZINGATIA UADILIFU
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Mhe Harouna Ali Suleiman amezitaka Madrasa za Dini kusimamia misingi ya Kiislam ili kutokomeza vizendo vya uhalifu.
Akifunga Mafunzo ya Walimu wa Madrasa ya Elimu ya Amali Waziri Haroun amesema misingi ya Dini iliyobora humjenga Mwanafunzi kuwa na Muongozo mwema katika Uislamu hivyo ni vyema kuhakikisha Mafunzo hayo yanaleta tija kwa Walimu.