SMZ IMEOMBWA KUWEKA KODI RAFIKI KWA WAJASIRIAMALI LIMBANI.
Wafanyabiashara katika Soko la Wajasiriamali Limbani Wete, wameiomba Serikali kuweka Kodi rafiki pamoja na kusimamia mnada wa Bidhaa Sokoni hapo ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata Wanunuzi.
Wametoa ushauri huo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Wete Dkt Hamad Omar Bakar ya kuangalia mwenendo wa Biashara katika Soko hilo.
Wamesema maendeleo ya Biashara zao zinakwamisha kutokana na kodi na kushindwa harakati zao za kujiongezea kipato.