DKT.NCHIMBI AAGIZA KUFANYIKA UTAFITI SEKTA YA MISITU

DKT.NCHIMBI UPANDAJI MITI
English

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emanuel Nchimbi, ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori) kufanya utafiti utakaosaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili Wakulima wa Miti, hususan katika mMsitu ya asili.

Dkt. Nchimbi ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani pamoja na Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji Miti iliyofanyika katika Manispaa ya Lindi, Mkoani Lindi.

Amesema Kampeni hiyo ya upandaji Miti ni Sehemu ya juhudi za Serikali katika kulinda na kuhifadhi misitu, pamoja na kuongeza uwajibikaji katika uhifadhi wa mazingira

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, maarufu kama Ashatu Kijaji, amesema kuwa Kampeni ya “27 ya Kijani” imekuwa chachu muhimu katika kuongeza mwamko kwa Watanzania kushiriki katika upandaji miti na uhifadhi wa mazingira.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, amesema kuwa kutokana na umuhimu wa Mikoko katika Ikolojia ya Bahari na mazingira kwa ujumla, Mkoa huo umeendelea kuratibu uhifadhi wa miti hiyo, ambapo Jumla ya Hekta 27,660 za Mikoko zimehifadhiwa hadi sasa.

Aidha, Mratibu wa Miradi wa Shirika la Earthlungs, Husen Hassan, ameeleza kuwa Shirika hilo limejikita katika upandaji wa Mikoko katika Mikoa ya ukanda wa Pwani kutokana na mchango wake mkubwa katika kulinda mazingira ya bahari na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.