JESHI LA POLISI LAHIMIZWA KUONGEZA UFANISI KATIKA KAZI ZAO

KUKABIDHIWA NISHANI JESHI LA POLISI

    Kamishna wa Polisi Zanzibar  Hamad Khamis Hamad amewataka Watendaji wa Jeshi la Polisi sifa wanazozipata za ufanyaji kazi bora ziendane na huduma bora katika kuwatumikia Wananchi.

    Akikabidhi Nishani kwa  Wakaguzi na Askari 20 wa Vitengo vya Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,

   Kamishna  Hamad  amesema  ari ya uwajibikaji uende sambamba na kuondosha Kero za Wananchi wanapofuatilia haki zao kupitia vyombo vya sheria.

   Kamishna msaididi Mwandamizi wa Polisi  Ngoi  amesema Nishani na Zawadi wanazopewa Askari wa Jeshi la Polisi itakuwa ni chachu ya kufanya kazi kwa kuzingatia haki, weledi, uaminifu na nidhamu

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.