Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali Mhe Ali Abdulgulam Hussein amewahimiza Wajumbe wa Bodi ya Usimamizi wa Mikopo ya Elimu juu kusimamia haki na uadilifu kwa kuhakikisha Mikopo inatolewa kwa walengwa.
Akizindua Bodi Mpya ya Usimamizi wa Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar yenye Wajumbe 7 chini ya Mwenyekiti wa Profesa Mohammed Hafidh amesema kufanya hivyo kutasaidia Vijana wengi wa Zanzibar wenye sifa na vigezo kufikia lengo na dhamira ya Serikali kwa Vijana katika kupatikana Wataalamu wa fani mbalimbali Nchini. Hivyo ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha dirisha la udahili kuwa wazi wakati wowote katika kusaidia Vijana.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wajumbe waliomaliza muda Makamu Mwenyekiti Mstaafu Bi Rabia Abdalla Hamid amesema kwa Kipindi chao cha Uongozi Bodi hiyo ilisimamia vyema Majukumu yake na kuitaka Bodi hiyo Mpya kuiga Mfano huo ili kufikia malengo.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bw.Khamis Abdalla Said amesema katika Kipindi kilichopita Bodi imeweza kuvuka malengo kwa kutoa Mikopo mingi.