Mahakama Kuu ya Tanzania na Kampuni ya M/S Deep Construction Limited ya Morogoro imetiliana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Kituo Jumuishu cha utoaji haki Kisiwani Pemba.
Akizungumza mara baada ya kuweka Saini hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mhe.Kai Bashiru Mbarouk amesema Kituo hicho kitakuwa na mazingira bora ya utendaji kazi na kuwapunguzia shida Wananchi wa Kisiwa cha Pemba kufuata huduma za Kimahakama katika Maeneo ya mbali
Aidha Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mheshimiwa Profesa Elisante Ole Gabriel amesema Ujenzi wa Kituo hicho unatokana na Mashirikiano kati ya Serikali ya Muungano na Zanzibar katika kutoa fursa katika kupatikana huduma jumuishi ili kupatikana haki kwa Wananchi Kisiwani Pemba
Katika Hafla hiyo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla amesema kuwepo kwa Kituo hicho ni Jambo la Kihistoria kwa Zanzibar ikiwa ni katika kudumisha Muungano wa Tanzania.
Mkandarasi wa Ujenzi huo kutoka Kampuni ya M/S Deep Construction Binda Singh Jabal amesema kwa mashirikiano kati ya Mahakama na Wananchi watahakikisha Mradi huo unakamilika kwa wakati
Ujenzi wa Kituo cha Kituo Jumuishu cha utoaji haki Kisiwani Pemba unatarajia kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni Tisa hadi kukamilika kwake.