MAAFISA MANUNUZI WATAKIWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

Maafisa manunuzi

    Jaji Dhamana wa Mahakama kuu Zanzibar,Kisiwani Pemba,Salim Hassan Bakari amewataka Maafisa Manunuzi,na Wahasibu kuwa waadilifu kwa kutojihusisha na Rushwa na badala yake kusimama imara katika kupiga vita vitendo hivyo kwenye  utekelezaji wa majukumu yao.

    Jaji Dhama ametoa  kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa Manunuzi Wahasibu na Wanasheria katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Sheria za Manunuzi huko makatiba kuu ya Chake Chake.

    Amesema  katika sehemu ya Manunizi  kumekuwa kukijitiokeza  vishawishi vingi vya Rushwa na ufisadi katika kufanya manunuzi jambo linaloweza kuisababishia hasara Serikali hivyo aliwataka Maafisa hao kusimama imara katika kupiga vita adui huyo.

     Aidha Jaji huyo aliwaomba Maafisa hayo kuangalia sheria ambazo zinakwanza katika utekelezaji wake ili ziweze kufanyikwa marekebisho.

     Mapema Mratibu wa Mafunzo hayo amesema  ni sehemu wa kuchochea uwajibikaji,uwazi na kuwajengea uwezo kwa kufanya kazi zao kwa weledi huku yakiwashirikisha Maafisa manunuzi Wahasibu na Wanasheria.

     Mafunzo hayo ya Siku Saba yaliwashirikisha Maafisa Wahasibu na Wanasheria wa Taasisi mbali mbali za umma Kisiwani Pemba.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.