KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA KUPUNGUZA VIHATARISHI VYA MAAFA NCHINI

KAMATI YA KUSIMAMIA MAAFA NCHINI

Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeihimiza  Kamisheni ya kuakbiliana na  Maafa Nchini kuendelea kuweka Mikakati Madhubuti katika kujiandaa na kukabiliana na maafa pindi yanapotokea ili kupunguza vihatarishi vya maafa Nchini.

Wajumbe wa Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe Machano Othman Said wametoa ushauri huo wakati wakipokea Taarifa ya  Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wete Pemba.

Wameikumbhusha Kamisheni ya kukabiliana na Maafa umuhimu wa kujiandaa na kukabiliana na Maafa kwa kuzingatia Madhara yanayotokea pamoja  na kufahamu Wajibu wa kila mmoja katika Eneo la kazi kuendelea kuchukua hatua stahiki endapo  Maafa yanapotokea  ili kuokoa Maisha na Mali za Jamii kutokana na Matukio hayo.

Nao Viongozi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wakiwasilisha  Taarifa ya utekelezaji wa Wizara hiyo wameihakikishia Kamati KWAMBA  Wizara inaendelea kujipanga katika kufanyia kazi  maelekezo yaliyotolewa na Kamati hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa tahadhari za mapema ili kuendelea kuwa na nguvu ya pamoja katika kukabiliana na Maafa Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.