KAMPUNI YA NOHA YAPELEKA FURAHA KWA HUYU MAMA

Mama wa mtoto mwenye ulemavu na waziri Pembe

    Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto  Mhe.Riziki Pembe Juma amekabidhi Nyumba Mama wa Mtoto mwenye ulemavu mchanganyiko Abdilah Kassim, ili kumuondelea shida ya makazi  

   Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyumba iliyojengwa na Ttaasisi ya NOHA amesema  Serikali kwa kushirikiana na Taasisi hiyo imeona ipo haja ya kufanya hivyo ili kumpunguzia usumbufu aliyokuwa akiupata hivyo amemuomba Mama huyo kuitumia Nyumba hiyo kwa malengo yaliokusudia ili kujenga uaminifu kwa Wafadhili hao kuendelea kuisaidia Jamii

    Mkurugenzi wa Taasisi ya NOHA  Mama Park amesema Taasisi  yake itaendelea kustawisha  maisha ya Jamii  ya Wazanzibari wakiwemo wenye ulemavu na wenye  hali ngumu za kimaisha  ili  kuyainua makundi hayo  

    Mkurugenzi  Ustawi wa Jamii na Wazee Mwalim Hassan iIbrahim wameitaka  Jamii hasa akina Baba kuacha tabia ya kuzitelekeza Familia zao pindi wanapopata Watoto wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu 

    Mama mzazi wa  Mtoto mwenye ulemavu Ndg.Siti  Khamis Rashid ameipongeza Serikali na Taasisi ya NOHA kwa  juhudi zao na kuahidi kuitumia msaada huo kwa malengo yaliokusudia .

    Zaidi ya Shilingi Milioni 25 zimetumika kujenga Nyumba hiyo ikiwa ni msaada kutoka Taasisi ya NOHA

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.