WANAWAKE WAMETAKIWA KUA MSTARI WA MBELE KUTANGAZA MAENDELEO YANAYOTEKELEZWA NA SERIKALI.

UWT

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Sophia Simba kwenye kongamano la wanawake wa UWT Taifa la kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Sophia amesema, ni wakati wa Wanawake sasa kundi hilo likawa kinara katika kunadi maendeleo yaliyofikiwa pamoja na kupanga mikakati kwa ajili ya uchaguzi Mkuu mwakani.

Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwigelo na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Tunu Juma Kondo wamewasisitiza wanawake kushirikiana ili kuiimarisha Jumuiya pamoja na Chama.

Kongamano hilo lilojadili mchango wa Wanawake katika Mapinduzi lilikuwa na kaulimbiu ya “Tuimarishe Uchumi kwa Maendeleo ya Taifa”.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.