Ameyasema hayo katika Ziara ya kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa mabanda ya maonyesho huko Fumba, Waziri wa biashara na maendeleo ya viwanda, Mh Omar Said Shaaban amesema Wizara hiyo imetoa fursa kwa Wafanyabiashara kwa lengo la kuwainua wananchi wake kiuchum ili kuweza kuingiza pato la taifa
Amesema eneo hilo litakua na maeneo mbali mbali kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali sambamba na Ukumbi wa Kitaifa na Kimataifa kwa ajili ya Mikutano ya wadau tofauti.
Amewataka wananchi kutovunjika moyo kutokana na umbali wa eneo hilo na amewaahidi kuwaandalia mazingira mazuri ya miundombinu ya barabara.
stories
standard