Ametoa kauli katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi katika Mahanga ya Jeshi lakujenga uchumi JKU huko Chambani ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kilelecha maadhimisho ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, amesema pamoja na mahitaji yaliyoanishwa katika sheria ya 2003 ya Jeshi hilo kuwezakujiendeshe kiuchumi lakini Jeshi linapaswa kutumia taaluma ya ziada ili kwenda sambamba na mabadiliko ya Dunia.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Mahanga hayo Katibu Mkuu ofisi ya Rais tawala za Mikoa na idara maalum za SMZ Mikidadi Mzee amesema ujenzi wa Mahanga hayo umegharimu jumla ya shilingi zaidi ya shilingi Bilioni moja kutoka mfuko
Mkuu wa Serikali ambao utaweza kulisaidia Jeshi hilo katika utaoji wa huduma mbali mbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Matar Zahor Massoud, ameahidi kushirikiana na Viongozi wa kambi hiyo kuifanyia matengenezo barabara yakuelekea katika Kambi hiyo ili kulirahishia Jeshi hilo katika utekezaji wa majukumu yake ya kila siku.