MWALIMU AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE NA MWANAFUNZI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara

     Mwalimu wa kiume afahamikae kwa jina la Ramadhan Said Nanyalika (32) Mkazi wa Mtaa wa Matogoro, Tandahimba Mjini Mkoani Mtwara amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile, Mwalimu huyo amekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Naputa kwa kipindi kirefu sasa.

    Kamanda wa Polisi wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP, Issa Suleiman ametoa taarifa hiyo Julai 09, 2024

    Mwalimu wa kiume aitwaye Ramadhan Said Nanyalika (32) Mkazi wa Mtaa wa Matogoro, Tandahimba Mjini Mkoani Mtwara ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

    Taarifa hiyo imetolewa July 09,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP, Issa Suleiman, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya doria, misako, oparesheni na mafanikio ya Mahakamani kuanzia June 01, 2024 hadi June 3, 2024.

     “Mtuhumiwa siku za nyuma alijenga urafiki Shuleni na Mwanafunzi wa kiume wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kuanza kumnunulia vitafunwa Shuleni na kisha kumtaka Mwanafunzi huyo amtembelee nyumbani kwake, siku Mwanafunzi huyo alipomtembelea nyumbani, Mwalimu huyo alianza kwa kumuonesha video chafu kupitia simu janja yake (smartphone) na baadaye kumtaka amuingilie kinyume na maumbile”

     “Baada ya Mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho, ndipo Mwalimu alianza kumtisha kwa kumwambia endapo hatokubali kufanya hivyo atapata adhabu za mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kufukuzwa Shule, kutokana na Vitisho hivyo Mwanafunzi huyo
alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake na akamuingilia Mwalimu wake kinyume na maumbile” RPC Issa

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.