Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe.Sharif Ali Sharif amewataka Waumini wa Dini ya Kiislam kutoa mali zao na nafsi zao kwaajili ya kupeleka mbele harakati za Kiislam ili kuitengeneza Jamii yenye maadili mema .
Akizungumza katika Uzinduzi wa harakati za Ijitamia ya Kimataifa ambayo Mwaka huu inatarajiwa kufanyia Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Sharif amesema Taasisi za Kidini zina mchango mkubwa katika kuhuisha maadili mema katika Jamii .
Waziri Sharif pia amewasihi Viongozi wa Jumuiya ya Fisabilahiah kutumia Ijitmai hiyo kuwakumbusha Waumini juu ya umuhimu wa kuidumisha amani na utulivu uliopo Nchini
Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi ameisihi Jamii kufanya mambo ya kheri ili kupata radhi za Allah hapa Duniani na Akhera
Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'a' Othman Ali Maulid amesema Mkoa utaendelea kuunga mkono harakati za kufanikisha Ijitmai hiyo ikiwemo kuimarisha amani na utulivu .
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Fisabililah Tabligh Markaz maiyomba Jamii kuwa mstari wa mbele kushiriki katika harakati mbali mbali na ili kufanikisha Ijitmai hiyo ambayo inatarajiwa kukushanya Waislam kutoka Nchi mbali mbali za Afrika ya Mashairiki ikiwemo Kenya Uganda na Malawi
Katika Uzinduzi huo ulitanguliwa na Duwa maalum ya kumuombea aliyekuwa Kiongozi wa Jumuiya hiyo Sheikh Said Nyange aliyefariki hivi karibuni huko Saudia Rabia katika Mji Mtukufu wa Makka na Viongozi wengine waliotangilia mbele ya haki.