ZAIDI YA WANANCHI 2000 WANUFAIKA NA UJENZI WA ZAHANATI

ZAHANATI

   Zaidi ya Wananchi 2000 wa Kijiji cha Bugando na Vijiji vya Jirani Kata ya Chabula Wilaya ya Magu wameanza kunufaika na Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bugando iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kushirikiana na Wananchi ambao wamechangia Asilimia  10.

    Zahanati hiyo iliyojengwa na TASAF kwa gharama za Shilingi Milioni 93 imekamilika ikiwa na Vifaa vyote pamoja na Dawa..

    Ujenzi wa Nyumba  ya kuishi Watumishi wa Afya wa Zahanati hiyo ambayo ujenzi wake umefikia Asilimia 95 na Wodi ya Wazazi nayo ikiendelea kujengwa.
    Akizungumza Wakati wa Uzinduzi wa Zahanati hiyo  Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugando, Charles Methusela Kasuka amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo kutawaondelea adha ya kutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya katika Kata za Jirani.

   Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe. Boniventura Kiswaga ameishukuru Serikali   kwa kuendelea kutoa Fedha za kufanikisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Magu

    Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu, Eusebius Chanjali amewataka Wananchi wa Kijiji cha Bugando kutumia Zahanati hiyo kutatua shida zao  za kiafya na  kutoa ushirikiano wa Watumishi wa Zahanati hiyo 

  Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii  TASAF  Wilaya ya Magu , Daniel Samwel Sanyenge amesema Serikali  imejenga  Zahanati hiyo kutokana na uhitaji Mkubwa uliyopo kwa Wakazi wa Maeneo hayo ambao wanatembea umbali  mrefu kwenda Kata Jirani kufata huduma za Afya.  .

   Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Magu  Mohamed Ramadhani amewaomba  Wananchi kuendelea  kushiriki kikamilifu katika Ujenzi na Ulinzi wa Miradi inayojengwa na Serikali ili ilite tija iliyokusudiwa ya kutoa huduma. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.