Waumini ya Dini ya Kiislam wametakiwa kuhimizana juu ya umuhimu wa kutunza amani na utulivu ili kuendelea kuishi katika mustakbali mwema.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Hamza Hassan Juma katika Wiiki ya kuelekea kilele cha Mwaka Mpya wa Kiislam 1446 Hijria,
Amesema Uislam ni Dini iliyokuja kuondosha aina zote za Ubaguzi na ukandamizaji baina ya Watu, hivyo Waumini wa Dini ya Kiislam wanapaswa kujipambana na tabia njema ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wake Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shiekh Hassan Othman Ngwali, amewataka Wazazi na Walezi kushirikiana katika malezi ya Watoto wao ili kuepukana na vitendo vya uvunjifu wa Amani na kuwa na Jamii iliyobora.
Nae Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuidhinisha Sherehe za Mwaka Mpya wa Kiislam Kitaifa.