WAHANDISI ZHC WATAKIWA KUONGEZA UMAKINI KATIKA MIRADI YA NYUMBA

MKURUGENZI ZHC

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar Ndg.Sultan Said Suleiman amewahimiza Wahandisi wa Shirika hilo kuongeza umakini katika kusimamia Miradi ya Ujenzi wa Nyumba ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliopangwa.

   Akizungumza katika Nyakati tofauti Wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya ZHC na Maeneo ya Miradi mipya Ndg.Sultan amesema lengo la Ziara hiyo ni kuangalia na kufanya tathmini ya changamoto zilizopo katika Miradi hiyo ili kuendeleza juhudi za kuwapatia Wananchi Nyumba bora za Gharama nafuu.

   Aidha amesema Ziara hiyo ni chachu ya utekelezaji wa Azma ya Serikali ya Dkt.Mwinyi katika mkakati wa Mapinduzi ya Ujenzi wa Nyumba za Kisasa zikiwemo za Gharama Nafuu kwa Wananchi wa Maeneo mbali mbali Nchini.

   Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na uwekezaji ZHC Qs.Halima Bashiru Hassan amesema Shirika hilo limejipanga kuyaendeleza Maeneo yote ya Nyumba za Vijiji ili kufikia lengo la Serikali la kuwapatia Wananchi Nyumba bora na salama.

   Katika Ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar baada ya Mtangulizi wake kumaliza muda wake ametembelea Miradi ya Nyumba za Mombasa kwa Mchina, Mnadani, kwa Fundi Abduli, na Maeneo ya Miradi mipya ikiwemo Kisakasaka, Nyamanzi n Betrasi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.