KAMBI ZA MATIBABU ZA MARADHI MBALIMBALI HUSAIDIA KUIMARISHA AFYA ZA WANANCHI

MAKAMO WA KWANZA WA RAIS

   Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman amesema Serikali imekuwa ikishirikiana na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya ili kuona kunapatikana huduma bora kwa Wananchi

    Akifungua Mkutano Mkuu wa Wataalamu wa Ugonjwa wa Macho Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar amesema kupitia Mfumo wa Mashirikiano kati yao kumekuwa na ongezeko la Kambi za Matibabu ya Magonjwa mbali mbali na kuongezeka tafiti za Magonjwa yanayoathiri Jamii

    Amesema Serikali imekuwa na mipango ya kukuza huduma kwa mujibu wa malengo ya Dunia kwa kuweka Vipaumbele katika huduma za Matibabu hivyo hatua hiyo pia itasaidia kubadilishana uzowefu na Madaktari Bingwa pamojaa na kuwaongezea Ujuzi Madaktari wa Ndani

   Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara itashitikiana na Chama cha Madaktari wa Macho katika kutafuta namna bora ya kutibu matatizo ya Macho kwa kuwa na Vifaa vya Kisasa na kuomba Vijana kusoma Udaktari wa Macho ili kuongeza Wataalamu 

   Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dk.Christopher Mwanansao amesema lengo la Chama hicho ni kushirikiana na Serikali katika kutoa Matibabu ya Macho ikiwemo kufanya tafiti hasa baada ya kugundua kuwepo idadi kubwa ya Ugonjwa wa Presha ya Macho

    Mkutano huo wa Tano uliofanyika kwa Mara ya Kwanza hapa Zanzibar umetanguliwa na Kambi Maalum ya Siku Tatu kwa ajili ya kutoa Matibabu ya Macho ambapo Watu wapatao Elfu 1 na 15 Walichunguzwa  na 168 Walifanyiwa Upasuaji

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.