Akizindua Bohari ya kupokea na kuhifadhia Gesi ya Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited huko Mangapwani amesema utekelezaji wa Mradi huo utawezesha kupokea Meli kubwa zenye kukidhi mahitaji ya Nchi kwa zaidi ya Miezi Mitatu bila ya tatizo na kuwezesha kuimarisha shughuli za kiuchumi, kijamii na Maendeleo ya Miundombinu na kupunguza Msongamano wa Gari zinazobeba Mafuta na Gesi, Gari za Abiria na Mizigo Barabarani.
Katika hatua nyengine Dkt.Mwinyi amewatoa wasiwasi na kuwaahidi Wananchi wa Mangapwani na Bumbwini kuwa wote watakaoathiriwa na Uwekezaji wa Mradi huo katika Eneo hilo watapatiwa Fidia stahiki ili kupisha utekelezaji wake.
Nao Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ZURA Bw.Omar Ali Yussuf wamesema wataendelea kusimamia sheria na miongozo ya Serikali ili Eneo hilo liwe kuu la usambazaji wa Huduma ya Gesi ikiwemo Afrika Mashariki.
Mweneykiti wa Kampuni ya Vigor Mhe.Tawafiq Salim Turky na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Bw.Benoit Araman Turkey ameahidi kuendelea kutoa huduma kwa Watanzania ili kuleta Maendeleo.