Wizara ya Fedha na Mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupokea Euro Milioni 3 kutoka Taasisi ya Giz`3 ya Ujerumani zitakazo saidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya Maji Visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa (SMZ) Dkt.Juma Malik wakati wa hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa Maji na Taasisi ya Giz yaliyofanyika Jijini Dar-es -salaam.
Katibu Mkuu Dkt.Juma Malik amesema Mkataba wa Mradi huo upo katika hatua ya Awali ya Mazungumzo na Benki ya Ujerumani katika kuhakikisha wanawapatiapa Fedha zaidi.
Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini wa SMZ) Ndg.Joseph Kilangi amesema Mkataba wa Mradi huo utasaidia kuimarisha huduma za Maji hususan katika kutunza vyanzo vya Maji.
Meneja wa Maji wa Taasisi ya Giz Thobias Godau amesema wanaunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utoaji wa Huduma za Maji utakao warahisishia Wananchi wa Zanzibar.
Mradi unalenga kuimarisha upatikanaji wa Huduma za Maji Visiwani Zanzibar Aidha Mradi huo ni wa Miaka 3 na unatarjiwa kuaanza Mwezi Julai 2024 Hadi Julai 2027,