NYUMBA ELFU TATU ZA BEI NAFUU ZATARAJIWA KUJENGWA KATIKA ENEO LA CHUMBUNI

UTIAJI SAINI

   Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imetiliana Saini na Kampuni ya Weihai Huatan kutoka China kwa lengo la Ujenzi wa Nyumba za Bei nafuu  ambazo zinatarajiwa kujengwa Eneo la Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibi.

   Akizungumza mara baada ya Utiaji Saini huko Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mhe Salha Mohammed Mwinjuma amesema hatua hiyo itasaidia kuondokana na matatizo ya upatikanaji wa Maakaazi kwa Wananchi ambapo Ujenzi wa Nyumba hizo umekusudia zaidi kwa Wananchi wa Kipato cha chini.

    Mwenyekiti wa Kampuni  ya Weihai Huatan Xiangua Wang ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wanaoupata pamoja na Wizara ya Ardhi na kuahidi watahakikisha Ujenzi huo utakamilika kwa Wakati.

   Jumla ya Nyumba Elfu Tatu(3000)zinatarajiwa kujengwa katika Eneo la Chumbuni ambapo kwa upande wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mkataba huo Umetiwa Saini na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe:Salha Mohammed Mwinjuma na kwa upande wa Kampuni ya Weihai Huatan umewakilishwa na Xiangua kutoka China.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.