Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar Mhe.Shamata Shaame Khamis amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau mbali mbali katika kukuza Sekta ya Kilimo kwa manufaa ya Wananchi na Taifa .
Mhe.Shamata amesema hayo wakati alipokuwa akizundua Kituo cha Elimu ya Vitendo kwa Wakulima( Agro Connect ) huko Kangagani Pemba
Mhe.Shamata amewataka Wakulima kukitumia Kituo hicho kwa kupata elimu ili waweze kubadili melekeo wa Kilimo na kulima
kilimo chenye tija huku wakipata chakula cha uhakika.
Akizungumza katika Hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk Khatib amewataka Wakulima kufuata
maelekezo wananayopewa na Wataalamu wa Kilimo kwa lengo la kuimarisha Kilimo chao pamoja na Kulima Kilimo kinachoendana
na Wakati.
Nae Mkurugenzi Trias Afrika Mashariki Bibi Anna Constantine amesema wameona ipo haja ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar katika kutoa Elimu kwa Wakulima ili kuwakuza kwa kilimo kwa lengo la kuwainua hali zao Kiuchumi .
Kituo hicho ambacho kipo kwa majaribio kinaendeshwa na Taasisi ya Trias, Taha , Agri Connent kwa Mashirikiano na Wizara ya Kilimo na umoja wa Nchi za Ulaya Europian Union na tayari zaidi ya Wakulima Mia Tatu (300) wameshapatiwa Mafunzo.