WIZARA YA NCHI AFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO IMEPANGA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO YA SERIKALI

BARAZA LA WAWAKILISHI

Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango imepanga kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kutekeleza Bajeti yenye kuzingatia upembuzi yakinifu kuhusu uanzishaji wa Soko la Hisa pamoja na Benki ya uwekezaji Zanzibar .

Akiwasilisha hutuba ya makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka 2024/2025 Waziri wa Wizra hiyo Saada Mkuya Salum amesema Mpango huo unakusudia pia kuimarisha utoaji wa huduma kwa Wafanyabiashara Wadogo pamoja na ukusanyaji wa mapato katika Masoko mapya

Amesema Wizara itatoa vipaumbele katika kufanya tahmini ya utekelezaji wa Mpango wa maendeleo na kuanza maandalizi ya mkakati mpya wa maendeleo na Sera ya Viashiria vya Kiuchumi .

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Bajeti makamo Mwenyekiti wa Kamati Dkt Soud Nahoda Hassan ameiomba Serikali kuipatia Fedha kwa mujibu wa Bajeti hiyo pamoja na kupatiwa Wataalamu wa kuendeleza Wafanyakazi kwa kuwapatia nyenzo za kufanya utafiti

Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Wizara hiyo imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni Mia Nne kwa ajili ya utekelezaji wa matumizi mbalimbali ya Wizara hiyo

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.