Wafanyabiashara wanaoleta Bidhaa kutoka Nje ya Nchi wametakiwa kuhakikisha Bidhaa hizo zinakidhi vigezo na masharti ili kuweza kukuza Soko Kitaifa na Kimataifa.
Akizungumza katika Mkutano wa Waingizaji wa bidhaa za Uchapishaji Afisa Viwango Kemikali ZBS ,Ndg.Thahiri Khelefu Ali Amesema hivi sasa kumekuwa na bidhaa nyingi kutoka Nje zisizokuwa na Vigezo hivyo amewataka Waingizaji hao kuhakikisha Bidhaa wanazoingiza zinakizi Vigezo ili kuepusha gharama na usumbufu kwa Watumiaji wa Bidhaa hizo.
Nao Washiriki walioshiriki katika Mkutano huo wamesema Watayafanyia kazi Maagizo hayo na kuishauri ZBS kuweka Nembo katika bidhaa zilizo kaguliwa ili Wateja kupata Bidhaa zilizo bora na kukuza Uchumi wa Nchi
stories
standard