Makamo wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Isdori Mpango amekitaka Chama cha Wahandisi Washauri TAnzania ACET kuwandaa Wahandisi Washauri ili wawe na uwezo wa kusimamia Miradi mikubwa inayotekelezwa Nchi za Bara la Afrika.
Dr Philip mpango amesema hayo katika Kongamano la 3 la Shirikisho la Wahandisi Washauri lililofanyika Jijini Dar Es salaam ambapo amesema maendeleo ya Miundombinu ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya taifa lolote hivyo ni vyema Wahandisi wazawa wakajiweka vizuri ili kuweza kushindana na Wahandisi wa Kigeni.
Dr. Mpango amesisitiza umuhimu wa Wahandishi washauri wa Bara la Afrika kuwa na nguvu ya pamoja ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoikabili Sekta hiyo zikiwemo za kumaliza Miradi ndani ya muda uliopangwa na kwa kiwango kinachotakiwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesisitiza juu ya umuhimu wa Miradi mikubwa na ya kimkakati kutekelezwa na Wahandisi wa ndani ili Fedha zinatumika kwa utekelezaji wa Miradi hiyo zibaki hapa Nchini.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Charamila amesema muda umefika kwa Wahandisi kuzingatia Athari za mabadiliko ya Tabia Nchi katika Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ambayo imekuwa ikiathiriwa na mabadiliko hayo.
Kongamano la Shirikisho la Wahandisi Washauri Barani Afrika limewashirikisha Wadau mbalimbali kutoka chama cha Wahandisi Washauri Tanzania ACET na Shirikisho la Kimataifa la Wahandisi washauri FIDIC.