Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Khalid Salum Mohammed amewataka Wadau na Wasimamizi wa utoaji na usafirishaji wa Mizigo CAGO kuweka Mikakati itakayopunguza athari zinazosababisha Maafa na upotevu wa Mali.
Akifungua Mkutano wa Wadau wa usalama wa Anga na Wanaosafirisha na wanaotoa Mizigo katika Nchi za Afika Dkt Khalid amesema hivi sasa dunia inaenda Kidigitali hivyo usalama wa Mizigo ni muhimu ambapo Mafunzo hayo yatayawezesha kutambua wanaosfirisha mizigo kwa njia zisizo Halali.
Mkurugenzi wa huduma wa Udhibiti wa Usalama wa Anga Tanzania Salim Ramadhan Msangi amesema ifikapo Mwaka 2030 Nchi zote Wanachama wa Iq ni kupata zaid ya Asilimia 90 kwa vile lengo la Mkutano huo ni kuwaweka pamoja Washiriki wa Nchi 40 za Afrika ili kuzuia uhalifu wa Anga na kuwa salama.
Mkurugenzi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Seif Abdalla Juma amesema Serikali inahakikisha Sekta ya anga inafaidika na maendeleo hasa Usalama wa Anga na utoaji wa huduma mbali mbali.
Hannan Achahboun Meneja wa Mradi wa usafiri wa Anga wa Ulaya amesema lengo la kukutana pamoja kubadilishana uzoefu na kuwawezesha wanaotoa Mizigo kuongeza ujuzi katika kufanikisha kazi zao zinakuwa salama katika Viwanja vyote vya Ndege AFrika.
Mkutano huo umewashirikisha nchi 40 za Afrika ikiwemo TAnzania Kenya Uganda. Ethiopia na Malawi.