SERIKALI KUSHIRIANA NA TAASISI ZA DINI KATIKA KUSAIDIA HUDUMA ZA KIJAMII

ANGLIKANA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi za Dini kufanya shughuli zao kwa Uhuru na kushirikiana kutoa huduma kwa Jamii na kutatua matatizo yao.

   Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati wa Ibada Kuu ya Upatanisho na msamaha kutokana na madhila ya Biashara ya Utumwa iliyofanyika Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la Kikristo, Mkunazini na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Mhashamu Justin Welby.

    Dkt. Mwinyi ameridhia Ombi la Kanisa la Anglikana Tanzania la kutaka kuifanya Juni 6 ya kila Mwaka kuwa Siku maalum ya Kumbukumbu kuondolewa Biashara ya Utumwa na kuwashukuru Viongozi wa Dini kwa kuendelea kuhubiri amani, umoja na mshikamano.

   Katika hatua nyengine, Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imesamehe kodi ya makusanyo ya Watalii eneo la kihistoria la Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini, na kuitaka Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya kushughulikia kwa utaratibu mzuri wa makusanyo katika Eneo hilo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.