DKT.BITEKO AWATAKA WATANZANIA WASIKUBALI KUGAWANYIKA

Dkt.Biteko

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka Watanzania katu wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote na badala yake waulinde na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unatimiza miaka 60 ifikapo tarehe 26 Aprili, 2024 na serehe za maadhimisho yake yatafanyika Jijini Dar es Salaam.

    Dkt. Biteko amesema kuimarika kwa Muungano kumetokana na Amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania na hivyo Muungano ni moja ya Tunu za Taifa ambao unahitaji kulindwa ili kuenzi matunda yaliyopatikana. 

    Dkt. Biteko ameyasema hayo leo 20 Aprili 2024, mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Shehiya ya Kinyikani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

     "Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika na Duniani kwa ujumla kuwa na Muungano imara na thabiti kwa miaka mingi, hivyo ni vema kuulinda kwa namna yoyote ile" Alisema Dkt. Biteko 

     Awali, Dkt. Biteko alipata fursa ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kinyikani, kinachojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF)  na kusimamiwa na wakala wa ujenzi Zanzibar ZBA, ambapo hadi kukamilika kwake kituo hicho kitagharimu shilingi milioni 500.

      Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo zikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya, Shule na Miundombinu mbalimbali inatekelezwa.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.