Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mh Masoud Ali Mohammed, amewataka Wafanyabiasha waliopo katika Masoko ya muda, kuhamia katika Masoko mapya mara yatakapokamilika kujengwa.
Akizungumza na Kamati ya Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe ambayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni, ameagiza kupewa kipaumbele katika masoko mapya Wafanyabiasha waliokuwepo hapo awali na kufanya utaratibu wa kuwapatia nafasi Wafanyabiashara wengine.
Mh Masoud amezitaka kamati hizo kuwafahamisha na kutumia busara wakati wa kuwahamisha Wafanyabiashara hao katika maeneo ya Soko la muda Mwanakwerekwe C.
Aidha amezitaka Kamati hizo kukaa na wafanyabiashara kujadiliana juu ya maendeleo ya Masoko mapya ili yaweze kutoa huduma za mahitaji kwa ufanisi zaidi.
Wajumbe wa kamati ya Soko la Mwanakwerekwe na Jumbi, wamependekeza Masoko hayo yaendeshwe kibiashara ili yaweze kutoa huduma vizuri na kuangalia uwezekano wa kupatiwa nafasi Wafanyabiasha ya Mitumba ambao wamekuwa ni sehemu ya watoaji huduma na wal