VIONGOZI WATOA MSAADA WA UJENZI WA MADRASA YA MPENDAE

VIONGOZI JIMBO LA MPENDAE

    Viongozi wa Jimbo la Mpendae  akiwemo Muakilishi Mhe.Shaabani Ali Muhammed  na Mbunge Ndg.Taufiki Salum Turkii  wamewataka Waislamu kutoa katika mambo ya kheri ili kupata radhi kwa mola wao .

    Wakizungumza katika hafla ya kukabidhi  mifuko ya Saruji miatatu kwa ajili ya Madrasa akiwa  huko katika Mskitini wa kwa Ameir Tajo wa Mpendae wamesema jambo hilo huleta mapenzi baina Watu Wa chini na wenye uwezo.

    Wamesema viongozi hao kwa pamoja  wako tayari kutoa kwa mujibu ya mahitaji ya  Wananchi wa Jimbo kwa shughuli zote za maendeleo.

    Wananchi na Maimamu wa Mskiti wa Shekh Ameir Tajo wa Mpendae wamewa shukuru  Viongozi wao wa Jimbo kuendeleza kuwasaidia ujenzi wa Madrasa yao na kuwasihi Viongozi wengine  kuchangia pale palipo bakia.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.