Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh Ana Atanas Paul amesema kuwepo kwa Misaada mbalimbali ya kuwasaidia Watoto Yatima na Wazee ni Alama ya Imani na Ushirikiano kwa Watu hao.
Akikabithi Msaada wa Chakula kwa Niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika Vituo vya kulelea Watoto Yatima na Wazee wasiojiweza amesema Serikali inatambua Thamani ya Makundi hayo katika kuwawezesha kwa kuwapatia Msaada stahiki katika Vituo vyao.
Aidha ametoa Salam za Mama Mariam Mwinyi amesema Msaada huo wa Chakula ni ishara ya kuwanao pamoja katika kuwafutarisha Mwenzi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Nao Wananchi waliopokea msaada huo wamemshukuru Mama Mariam kwa kwa Sadaka hiyo na kutoa Wito kwa Waumini wengine kutoa Misaada mbalimbali kwa Wananchi.
Jumla ya vituo vitano vimepatiwa Msaada huo ikiwemo Kituo cha kulelea Watoto ya Tima Mazizini na Nyumba za Sebleni.