Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuendelea Kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa matendo mema kwa Watanzania na amesema Serikali itaendeleza yale aliyoyaacha.
Amesema hayo katika Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mt. Yohana Maria Muzeyi Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela na Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe.Medadi Kalemani wamemzungumzia Hayati Magufuli kwamba alikuwa Kiongozi maghiri na Mtu wa Watu.
Awali Familia ya Hayati Dkt.Magufuli katika Misa hiyo waliwashukuru Watanzania kwa kumkumbuka Mpendwa wao.
stories
standard