RC AYOUB ATAKA SHEREHE ZA MWAKA KOGWA KUTANGAZWA KIMATAIFA

Mwaka kogwa

    Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja  Ayoub Mohammed Mahamoud ameitaka Kamati ya Sherehe za Kijadi za Mwaka Kogwa  kuzitangaza Sherehe hizo Kimataifa  ili zilete tija  kwao na kwa Taifa.

    Akizungumza na Wazee wa Kamati ya Mwaka Kogwa Makunduchi Mkuu huyo wa Mkoa amesema  Tamasha hilo la muda mrefu lakini halijatangazwa kama yalivyo Matamasha mengine Duniani.

    Amesema kuendesha Tamasha la Mwaka Kogwa kimazowea halitawaletea tija hivyo ameitaka Kamati hiyo kuleta Mageuzi pamoja na  kujifunza kwa Mataifa mengine ili kuhakikisha linakuwa kivutio zaidi kwa Wageni.

    Mwenyekiti wa Kamati  hiyo Ndg.Mwita Masemo ameiomba Idara ya Makumbusho na Mambo ya kale kuangalia uhalisia wa jiwe lenye kusadikiwa kuwa na muonekano wa Ramani ya bara la Afrika ili liweze kuwa ni sehemu ya Kivutio cha Utalii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.