MABADILIKO YA KASI YAHITAJIKA PBZ

UTAMBULISHO NAIBU WAZIRI

    Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, imeitaka Benki ya Watu wa Zanzibar Pbz kubadilika ili kwenda kwa kasi zaidi na kufikia malengo ya Serikali.

    Akijitambulisha kwa Uongozi wa Benki ya Pbz Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juma Makungu Juma amesema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana na Benki hiyo bado ipo nyuma katika utoaji wa huduma ukilinganisha na Benki nyengine zilizoanzishwa hivi karibuni ambazo zinaonekana kuwa juu.

    Aidha amesema lengo la Serikali la kuanzisha Benki hiyo ni kuhakikisha inafanya kazi katika kuwahudumia Wateja na kujiendesha kibiashara.

    Naye, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Pbz, Ndg.Said Mohammed Said, ameahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kupiga hatua za kusimamia miakakati yake ili kuona inatoka kuwa Benki ya Saba na kuwa Benki ya Tano.

    Wafanyakazi wa Benki hiyo wameiomba Serikali kuendelea kuipa nguvu na kuyapatia ufumbuzi baadhi ya matatizo wanayokumbana nayo katika kazi zao.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.