Waziri wa Nchi afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohammed, amewataka Wakandarasi wa Ujenzi wa Maduka ya Darajani, kulifanya eneo hilo kuwa kivutio kwa Watumiaji.
Akikagua Ujenzi wa Maduka unaoendelea wa Awamu ya Pili wa Darajani Souk, unaejengwa na Kampuni ya Simba Developers, amewataka kuhakikisha kuwa Ujenzi huo unakamilika kwa wakati na ubora ili kuweka Mji katika Mazingira mazuri.
Mkuu wa wilaya Mjini Rashid Simai Msaraka, amesema Ujenzi huo unazingatia Wafanyabiashara wa aina zote ikiwemo kuwatengenezea maeneo rasmi Wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuweza kukuza kipato chao na kuchangia pato la Serikali.
Nae Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Simba Developers, Idris Noorani, amesema Ujenzi huo upo katika kiwango cha kuridhisha ili Wananchi waweze kunufaika na Mradi huo.
Mradi huo umejumuisha Milango ya Maduka, Migahawa na Maegesho.