Wananchi wa Shehia ya Makombeni Wilaya ya Mkoani wameishukuru Taasisi ya Waterfall Charity kwa kuwapatia msaada wa Vyakula mbalimbali kwa ajii ya maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Shukrani hizo zimetolewa mara baada ya kupokea msaada huo huko Kiwanja cha Mpira wa miguu Makombeni.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja akizungumza na hadhara hiyo ameishukuru Taasisi hiyo kwa uwepo wao katika Shehia ya Makombeni, kwa kuona umuhimu wa Mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu, huku akiwaomba Wanamakombeni kuitumia fursa iliyopo, ambayo italeta tija kwao na taifa kwa jumla.
Naye Meneja wa Jumuiya hiyo Tanzania Ndg. Mohamed Makame amesema Jumuiya yao imekuwa ikisaidia huduma mbalimbali katika Jamii ya Tanzania, kwa lengo la kuimarisha maendeleo yao.
Jumla ya Familia MiaTatu na Ishirini na Mbili, zimefaidika na msaada huo wa Chakula kutoka kwa Taasisi ya Waterfall Charity, ambayo Makao Makuu yake yapo Nchini Uingereza, ambapo katika hafla hiyo pia Jumla ya Watu Kumi na Nane wameweza kuchangia damu salama.