SMZ KUSHIRIKIANA NA WADAU WA UTALII KUKUZA SEKTA YA UTALII

WAZIRI WA UTALII NA MAMBO YA KALE ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Wadau wa Utalii ili kukuza Sekta ya Utalii Zanzibar.

Akizungumza katika Kikao cha Wadau wa Utalii Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe Mudrik Ramadhan Soraga amesema hatua hiyo itasaidia kukuza Uchumi wa Nchi na kuleta Maendeleo kupitia Sekta hiyo na kuona Utalii unainufaisha Zanzibar katika Nyanja mbali mbali. 

Waziri Soraga amesema atahakikisha Wanashirikiana na ZRA kuimarisha mifumo ya malipo kwa Kielektroniki yanafanyika ili kuongeza Pato la Serikali.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Zanzibar Ali Amour amesema lengo la Kikao hichi ni kujadili matatizo mbali mbali kuyatatua ili kuhakikisha Utalii unakua na kuengezeka kwa Wageni Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.