SERIKALI ZOTE MBILI ZINAUNGA MKONO JUHUDI ZA SEKTA BINAFSI.

DR KHALID SALUM MOHAMMED

Waziri wa Ujenzi  Mawasiliano na Uchukuzi Dr Khalid Salum Mohammed  amesema Serikali zote mbili zinaunga Mkono juhudi za Sekta Binabsi kwa kuendana na Sera za Serikali katika kufikia mabadiliko ya Kidigitali.

Akizungumza katika Hafla ya Uzinduzi wa ushirikiano  wa Kidigitali baina ya Kampuni ya simu ya Airtel Money  na Zanzibar Cable Televition  Dr Khalid amesema  juhudi za Sekta Binabsi zinaakisi vipaumbele vya Serikali ikiwemo Uchumi wa Blue  Utalii na uunganishaji wa Miundombinu ambayo vinategemea mabadiliko ya Kidigitali ili kufikia maendeleo endelevu.

Mkurugenzi Airtel Money  Andrew Rugwamba amesema wanarahisisha huduma kwa Wateja pamoja na kukuza uchumi na Biashara ili kuhakikisha mpango huo unafikiwa.

Mariam Mwamnyalla Meneja huduma za Airtel Money amesema wanatoa huduma za Kifedha katika Nchi 14 na Mawakala 220 kwa Nchi nzima kwa kutumia  njia ya Teknologia ya kisasa.

Kaimu Mkurugenzi Zanzibar Cable Hafidh Kassim amesema wanatoa huduma kwa njia ya Air tel Money katika maeneo ya Zanzibar  kwa ushirikiano mzuri na Kampuni yenye ubia kwa Serikali na Airtel Money na Zanzibar cable.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.