TAKUKURU YABAINI KASORO MIRADI KINONDONI

TAKUKURU

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni imebaini kasoro katika Miradi minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni 7 nukta 2 katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar- es-salaam.

   Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Ndg.Ismail Suleiman wakati akitoa Taarifa ya Utendaji wa Taasisi hiyo katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023.

   Amesema pia wamebaini Kampuni iliyopewa Jukumu la kukusanya Ushuru katika Masoko ya Manispaa ya Kinondoni ilikuwa inafanya udanganyifu wa ukusanyaji Mapato pamoja na kuwasilisha kiasi kidogo cha pesa Benki 

    Aidha Ndg.Selemani amesema katika kipindi hicho jumla ya mashauri mapya matano yamefunguliwa hivyo kufanya jumla ya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa 20. Akitoa mikakati yaTaasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 Ndg.Seleman ameedelea kwa kusema.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.