Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,amesema Serikali inadhamiria kuongeza mikakati ya kulinda mazingira ili kukabiliana na ongezeko la Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Saratani.
Akizungumza katika Kikao cha uwekezaji wa Sekta ya Afya kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Saratani Nchini huko katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar- es- salaam, amesema Saratani ni Ugonjwa unaowaathiri Watu wengi Ulimwenguni.
Amesema lengo la kukuza Mazingira ni muhimu katika kuwavutia Wawekezaji wa ndani na wa Kimataifa, hivyo uwekezaji katika huduma za Saratani unakusudia kujenga matumaini ya maisha ya Watu ambao wamekumbwa na maradhi ya Saratani.
Dk. Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mtu anayekutana na tatizo la Maradhi hayo anapata huduma kamili ya matibabu stahiki
Amesisitiza kuongeza nguvu katika rasilimali fedha ili kuimarisha utafiti, kuimarisha Miundombinu ya Afya, na kuhakikisha upatikanaji wa matibabu bora kwa Wagonjwa wa Saratani kwa Nchi nzima. amesema Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi, Watafiti na Wataalamu wa Tiba, Tanzania inawezekana ikabadilisha muonekano wa huduma za Saratani.
Awali Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali ilikuwa inatafuta Miundombinu kukamilisha mpango huo.