UJENZI WODI YA WAZAZI KATA YA MNALI MANISPAA YA LINDI KUANZA

UJENZI WODI

    Wananchi wa Kata ya Mnali Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wameishukuru Serikali kwa kuanza Ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Kata hiyo.

    Hatua ya Serikali kujenga Wodi hiyo  imekuja baada ya kuwa na tatizo la ufinyu wa Chumba cha kujifungulia katika Zahanati hiyo  hali iliyowalazimu Wananchi kujitolea  kuanza kujenga Wodi ya Miti pembezoni mwa Zahanati hiyo  Mwaka 2022.

    Wakizungumza na ZBC Wananchi hao wamesema wanaipongeza Serikali kwa kuanza kuchukua hatua ya kujenga Jengo hilo ambapo kiu kubwa kwa sasa ni kuona Jengo hilo linakamilika na kuanza kutumika

    Dokta Wilfred Makomba ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mnali anaeleza jinsi wodi hiyo itakavyorahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma pindi itakapokamilika.

    Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Juma Mnwele amesema Ujenzi wa Wodi hiyo inajengwa kwa mapato ya ndani ambapo kwa awamu ya kwanza ulitengewa kiasi cha Shilingi Milioni 30 ambayo imefikisha jengo hilo katika hatua nzuri.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.