Serikali imesema itaendelea kuhakikisha Bidhaa na huduma za Bima mbalimbali zinapatikana Nchini hususani katika maeneo ya Vijijini lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma ya Bima Nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Saada Mkuya wakati wa Uziniduzi wa Kampuni ya Bima ya First United Takaful.
Amesema Serikali zote mbili zinaendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa Taasisi au Mtu anayetaka kufanya uwekezaji katika sekta ya Bima Nchini
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya First United Takaful Abdunasi Ali Mohamed amesema lengo la kuanzisaha Bima hiyo ni kuwafikia Watu wanaoamini misingi ya Dini ya Kiislamu katika suala ya Bima
Amour Muro ni Mkuu wa Idara inayotoa huduma za Kiislamu ndani ya Benki ya KCb Tanzania ambao ni miongoni wa Wadhamini katika uzinduzi huo ambapo alikuwa na hayo ya kusema.